Barua Ya Chahali

Share this post
Dear Mama @SuluhuSamia, Hawa Waliofoji Picha Hii Kwenye Gazeti la The Scotsman la Hapa Uskochi Wamekudhalilisha, Wachukulie Hatua
www.baruayachahali.com

Dear Mama @SuluhuSamia, Hawa Waliofoji Picha Hii Kwenye Gazeti la The Scotsman la Hapa Uskochi Wamekudhalilisha, Wachukulie Hatua

Evarist Chahali
Nov 3, 2021
Share

Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni janga la kitaifa. Huhitaji kuwa jasusi kama mie kubaini hilo. Ni janga la kitaifa kwa sababu lukuki, lakini ya msingi zaidi ni taasisi hiyo kuwa na watu wasio na akili (lack of intelligence) ilhali fani husika inahitaji akili kubwa kabisa. Na katika kuficha ukosefu huo wa akili, wahuni hao hukimbilia kwenye “ubunifu wa kupuuzi” kama ilivyothibitika tena jana.

Jana walitengeneza front page hii feki ya gazeti maarufu la The Scotsman

Baada ya uhuni huo wakawatumia watu wao kusambaza mitandaoni. Kilichofanyika ni kupandikiza hiyo habari feki ya Mama Samia kwenye toleo hili la mwezi Machi la gazeti la The Scotsman

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Dear Mama @SuluhuSamia umetuwakilisha vizuri #GlasgowCop26 lakini hao wahuni wa Idara ya Usalama wa Taifa wanazingua. Wameishiwa ubunifu hadi wanafanya vitu kipuuzi kama walivyofoji front page hii ya @TheScotsman 😡 Feki Halisi
Image
Image

November 2nd 2021

28 Retweets194 Likes

Kinachokera kuhusu tukio hili ni ukweli kwamba Mama Samia ametuwakilisha vema tu kwenye Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Athari za Mabadiliko ya Tabianchi. Sasa badala ya wahuni hao kuwekeza nguvu kwenye kunadi matukio halisi ya Mama Samia kuhusiana na mkutano huo unaofanyika hapa Glasgow, wao wakaona waibuke na huo uzishi usio na tija.

Kama unafutilia twiti zangu za hivi karibuni, nimejikita zaidi kwenye kufuatilia suala la ugaidi, hususan Msumbiji na DRC, na kila nafasi inaporuhusu, natupia jicho jinsi hali ilivyo kwenye nchi hizo inavyoweza kuwa na athari kwa Tanzania. Na moja ya vitu vya kutia shaka ni uwezo hafifu wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa kukabiliana na matishio halisi, na si ya kufikirika.

Ni matumaini yangu kuwa Mama Samia sio tu hatoruhusu uhuni wa ina hiyo kujirudia huko mbeleni bali pia atachukua hatua stahili dhidi ya waliohusika.

KAZI IENDELEE 😊

ShareShare
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing