Dear Mama Samia, CCM Inapata Wapi Mamlaka Ya Kutengua Amri Halali ya Polisi wa Usalama Barabarani Kuhusu Boadaboda Kuingia Mjini Kati Dar?

This sets a bad precedence. Katibu Mwenezi wa CCM anapoweza kutengua amri halali ya kisheria ya jeshi la polisi, ni hatari.

CCM yapiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia mjini

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeagiza marufuku ya waendesha bodaboda na bajaji kutofika au kufanya shughuli zao katikati jiji la Dar isitishwe mara moja kwa kuwa si muafaka lakini pia imetolewa kwa kukurupuka.

Kauli hiyo ya CCM imekuja siku moja baada ya Kamishana Msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Abdi Issango kunukuliwa akipiga marufuku bodaboda na bajaji wote kuingia mjini na wale walioko mjini watoke isipokuwa bajaji za walemavu. Marufuku hiyo ilikuwa ianze kutekelezwa rasmi tarehe 1 Novemba mwaka huu.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Oktoba, 2021, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema marufuku hiyo ilitolewa bila kuzingatia taratibu za msingi zinazopaswa kufanya uamuzi unaogusa masilahi ya wananchi.

Amesema jambo hilo limeleta taharuki na CCM imepokea kwa mshangao mkubwa kwani ni jambo ambalo halikuwa na matayarisho mithili ya watu kukurupuka katika kutoa maamuzi hayo.

“CCM kimepokea na kufuatilia malalamiko ya wananchi mbalimbali ikiwamo, machinga, waendesha bodaboda, sanjari na malalamiko hayo, CCM kinaungana na Rais Samia katika dhamira yake ya kuona nchi yetu inapangwa vizuri na kuwa kivutio kwa kuwapanga vema machinga na wafanyabiashara wengine.

“Tuliona sasa Rais amewajali na kuwathamini kwa kutoa maelekezo kwamba watoa huduma hizo wapangwe katika maeneo rafiki,” amesema.

Amesema Chama kimeagiza Mamlaka za kiserikali mkoa wa Dar es Salaam zinazohusisha viongozi na watendaji, vyombo vya dola na mamlaka zingine zenye majukumu ya kusimamia usafiri na usafirishaji maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam chini ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta hiyo, zikutane kwa haraka iwezekanavyo.

“Lengo ni kuangalia iwapo kuna changamoto zozote zilizojitokeza ili zijadiliwe na kupata ufumbuzi wa muda mfupi, wa kati na mrefu ama ufumbuzi wa kudumu ili kutoathiri na kubughudhi ustawi wa shughuli za makundi ya watu wanaohusika.

“Chama kinasisitiza kwa kuzingatia umuhimu wa suala hili, kitafuatilia na kuhakikisha

utekelezaji huu unafanyika kwa mafanikio makubwa,” amesema.

Na hatari hiyo sio tu katika kuingilia utendaji kazi wa watalaamu mbalimbali, kama hao wa usalama wa raia, bali pia inawavunja moyo watu wanaotekeleza majukumu yao na kuishia kuingiliwa na wanasiasa.

Lakini hatari zaidi ipo kwa Mama Samia mwenyewe. Sio siri kwamba yeye ndio amemuibua huyo Shaka na kumpa huo wadhifa mkubwa zaidi ya uwezo wake. Tunajua Shaka alikumbwa na kashfa ya ufisadi pale Morogoro na haikutegemewa angekuja kupewa wadhifa mkubwa kabisa ndani ya CCM. “Wanafiki” wanadai uzanzibari wake na ukaribu wake na Mama Samia ndo umemfikisha hapo.

Kuna ishara za awali za Shaka kugeuka “Bashite mwingine” kutokana na obsession yake ya kuingilia maamuzi halali ya serikali. Sawa, tunafahamu kuwa chama kimeshika hatamu lakini ni muhimu kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Kwa sababu, kinyume chake tunaweza kushuhudia kitu wanaita “domino effect,”

Imagine watumishi wa vyombo vya dola, au wengineo serikalini, au wananchi kwa ujumla nao waamue kufuata hicho anachofanya Shaka, tutaishia kuwa na lawless nation. Kwa sababu moja ya sababu kuu za nchi zisizotawalika kisheria ni sheria husika aidha kuonekana kama mzaha au hata zikiwa makini zinaishia kupuuzwa na takriban kila mtu.

Kama upo Twitter, angalia tweets zangu za “Lawless Nigeria (wakati mwingine badala ya neno Nigeria naweka tu alama ya bendera ya taifa hilo kubwa kuliko yote baranai Afrika), utaelewa athari za kuwa na “taifa lisilo na sheria,” yaani sio kama halina sheria as such bali kila sheria inaonekana kama a joke, mzaha.

CCM ni mabingwa wa kutengeneza matatizo na kujifanya wameyapatia ufumbuzi. Tatizo la bodaboda ni sehemu ndogo tu ya tatizo kubwa la usafiri wa uahkika sambamba na ukosefu wa ajira. Japo bodaboda zimeingia barabarani kuchangia sekta ya usafiri, lakini you and I know kuwa mapungufu kwenye sekta ya usafiri, hususan vijijini, yamelazimisha uwepo wa bodaboda. Kadhalika, bodaboda zimekuwa sio tu kitegauchumi bali pia chanzo cha ajira hivyo kuwezesha ujasiriamali.

Siku njema

TANGAZO:

Jiunge na Jarida la UJASUSI hapa