CCM Yasitisha Malipo Kwa "Watetezi wake Mtandaoni" aka "Lumumba Buku Saba" Kisa Korona 😍

Mtumishi wako kaiona habari hii huko Jamii Forums na akadhani ni vema akushirikishe. Hawa wahuni wa “Buku Saba Lumumba” wanatusumbua kweli mtandaoni lakini naona “korona imeingilia kati.” Classic case of “kufa kufaana.”😊

Ulipolileta wazo la kuanzisha 'Timu ya Utetezi wa CCM' mitandaoni katika vikao vya kichama ulisifiwa na wazo lako lako likapita. Vijana wakatafutwa na Timu husika ikaundwa ikiwa na jukumu kubwa la kutetea chochote kinachohusu Serikali au CCM au vyote viwili. Timu yetu ya mtandaoni ambayo humu JF imebatizwa jina la Lumumba Buku Saba inafanya vyema kutetea kwa kila uwezo wao. Kiukweli, hakuna jambo ambalo linahusu Serikali hii au CCM ambalo halisifiwi nao. Always, Lumumba Buku Saba wanakufa na tai zao shingoni.

Malipo ya Timu yetu ya Mitandaoni yanaratibiwa na Idara yako ya Uenezi na Itikadi ya CCM iliyopo chini yako Ndugu Humprey Polepole, muasisi wa wazo la timu husika. Pamoja na malalamiko na maombi ya wanatimu kutaka malipo yapandishwe kutoka elfu saba hadi kumi kwa siku, malipo yao yaliyokwishapitishwa kichama ya elfu saba kwa siku yamekuwa yakilipwa. Wanatimu wanajituma pamoja na kuwa ni wachache tu kati yao ndiyo waliowezeshwa kwa kununuliwa simu, tablet na kompyuta.

Malipo ya wanatimu yamesimama kwa muda sasa. Baadhi ya wanatimu wamenza kususa kwa ama kutoandika chochote mitandaoni au kuandika bila jazba, mihemko, hasira na kwa kejeli kama walivyoagizwa. Sababu zinazotolewa kuhusu kuyumba kwa malipo ya wanatimu ni kutokana na ugonjwa wa Corona. Vijana wanataka kujua, Corona imeathirije malipo yao? Ndugu Polepole kumbuka kuwa huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu. Tusiwaudhi wanatimu wa mtandaoni. Tuwallipe na kuwawezesha ili watusaidie.

Tuwe makini na ugonjwa wa Corona kwa kuchukua tahadhari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha, Tanzania)

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali