CCM Acheni Uhuni, Msiwe Watu wa Kutaka Sifa tu Ila Mkikosolewa Inakuwa Uhaini. Mama Samia ni Rais Wetu Sote, Sio wa Ninyi Wahuni Peke Yenu 😡

Jana nilitwiti kuhusu picha hiyo juu inayomuonyesha Rais Samia Suluhu akiagwa huko Misri na “waziri wa ngazi ya chini.” Niliandika

Twiti hiyo ilipelekea mashambulizi makali kutoka kwa baadhi ya wana-CCM. Sasa sijui walitaka hata penye walakini tukae kimya, au tusifie tu kwa vile hicho ndo wanachopenda kusikia - SIFA. SIFA. Na SIFA zaidi.

Na hii sifia sifia ya kizushi ndo imelifikisha taifa hapa pasipoeleweka kwa sababu hata mtu akifanya ufisadi, hao wahuni wa CCM watataka asifiwe hivyo hivyo.

Wamisri hawajamtendea haki Mama Samia. Angalau angeagwa na Waziri Mkuu lakini sio huyo junior minister. Sasa hata kuwakemea Wamisri kwa dharau hiyo nalo ni kosa?

CCM mnapaswa kuelewa kuwa Mama Samia ni Rais wa Watanzania wote ma sio wa ninyi wahuni pekee. Kadhalika, ili afanikiwe anahitaji sapoti ya Watanzania wote bila kujali itikadi zao, kwa sababu wana-CCM ni asilimia kiduchu tu ya Watanzania takriban milioni 60.

Lakini jingine, na hili ni la muhimu, mie binafsi ni sapota wa Mama Samia, japo nikiri kwamba kuna maeneo - kama kesi ya kionevu dhidi ya Mheshimiwa Freeman Mbowe - ananikwaza. Lakini kama nilivyotanabaisha mara kadhaa, we usually don’t easily give up on “good people” yaani kwa kawaida hatuwakatii tamaa watu wema mapema. Bado naamini huyo Mama ni mwema ila tu amezungukwa na maharamia wenye maslahi binafsi.

Nimalizie kwa kumkarinisha yeyote anayetaka kutumiwa kijarida cha Ujasusi, anaweza kujisajili hapa chini

JISAJILI NA KIJARIDA CHA UJASUSI