Catch-22: Mama @SuluhuSamia akitumia utu kumaliza kesi ya Mbowe atasutwa kuwa 'dikteta kasalimu amri.' Asipoingilia kati, ataendelea kuitwa 'dikteta.' Bora Jaji Tiganga aachiwe jukumu hilo
After all, kwa wafuasi wa Chadema, kila afanyalo Mama Samia ni baya 'by default', kwahiyo hakutokuwa na tija katika yeye 'kuingilia' kesi hiyo.
Ni wazi kuwa yote mema yaliyotarajiwa kufuatia mkutano wa kihistoria kati ya Mama Samia Suluhu na Tundu Lissu huko Brussels, Ubelgiji hapo Jumatano, yameelekea mtaroni.
Japo ilitarajiwa mapema kwamba ‘sehemu ya pili ya mlinganyo’ kuhusu mkutano huo wa Mama Samia na Lissu ingekamilika baada ya uamuzi wa Jaji Joachim Tiganda kuhusu iwapo Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu au la, kasi ya kuporomoka kwa matarajio ya mwafaka imekuwa ya kasi mno.
Ombwe la uongozi Chadema
Ukiongea na ‘wajuzi mbalimbali wa siasa za Tanzania’, watakwambia bila shaka kuwa ‘hakuna Chadema bila Mbowe.’ Na hilo linathibitika katika ombwe kubwa la uongozi wa chama hicho tangu Mbowe akamatwe na hatimaye kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi.
Moja ya sifa muhimu za Mbowe ni pamoja na kuwa na busara ya hali ya juu. Ukilinganisha kauli zake na za viongozi wengine wa chama hicho, hutoshindwa kubaini kuwa alikuwa makini sana katika kila alichoongea. Na hata pale alipoamua kuchukua msimamo mkali - kwa mfano chama chake kilipokuwa kililazimisha mkutano kati yao na Mama Samia - bado busara ilitawala ambapo alijiepusha na matumizi ya maneno makali au kauli za kumshushia heshima Rais.
Ni wazi kuwa laiti Mbowe angekuwa uraiani, asingekataa nafasi adimu ya kuruhusu utashi binafsi wa Rais utumike kumaliza kesi inayomkabili. Kwa sababu angetambua bayana kuwa moja ya mbinu muhimu za kisiasa ni pamoja na “kujifanya mjinga siku ipite.”
ACT-Wazalendo huko Zanzibar, walitumia busara kukubali “kujifanya wajinga ili siku ipite” baada ya kuridhia kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa na CCM ambayo serikali yake sio tu iliharibu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 bali pia ilisababisha vifo vya makumi ya wanachama wa ACT-Wazalendo na mamia ya majeruhi.
Japo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kutoka ACT-Wazalendo, amenukuliwa akisema kuwa hadi sasa mwafaka katika ya chama hicho na CCM haujazaa matunda yoyote, ukweli ni kwamba Zanzibar ina amani kuliko ilivyokuwa mara baada ya uchaguzi. Na amani hiyo ni matunda ya mwafaka baina ya vyama hivyo.



BBC News Swahili @bbcswahili
Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar asema hakuna hatua iliyofikiwa katika serikali ya umoja baada ya kifo cha Maalim Seif https://t.co/h0fjyhlBPJLicha ya Mbowe kusababishwa na Mbowe kuwa gerezani, ombwe la uongozi huko Chadema linachangiwa pia na kukosekana mamlaka ya kuongelea masuala muhimu kuhusiana na chama hicho.
Baada ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene, kujiengua kinyemelea, chama hicho kimekuwa na ombwe la “msemaji wa chama.” Japo Katibu Mkuu John Mnyika anaonekana kama anayeshikilia jukumu hilo kwa sasa, lakini misimamo ya chama imekuwa ikitoka takriban kwa kila anayejisikia kutoa tamko. Huku Lissu, kule Jon Mrema, hapa Godbless Lema, na kwingineko ni lundo na makada-wanaharakati wanaoamini kuwa idadi kubwa ya followers wao kwenye mitandao ya kijamii inawapa mamlaka ya kuwa wasemaji wa chama hicho.
Kwa upande mwingine, uwapo wa Lissu nje ya nchi nao umechangia kwa kiasi kikubwa tu uwepo wa ombwe hilo. Lissu sio tu ni kiongozi mwenye uzoefu bali pia bado ana mvuto mkubwa miongoni mwa wana-Chadema na Watanzania wengine kwa ujumla. Huenda kurudi kwake nchini Tanzania - kama alivyoahidi kwenye salamu zake za kuukaribisha mwaka 2022 - kunaweza kusaidia kuziba ombwe hilo la uongozi kwenye chama hicho.
Radical elements
Lilipotokea jaribio la Didier Abdallah Mlawa aka Kigogo la kutaka kupora uongozi wa chama hicho kuafuatia kukamtwa kwa Mbowe, ambapo mtu huyo alishauri Chadema “iunde jeshi lake…iingie mtaani”, Lissu alimshukia Mlawa “kama mwewe” na kumfahamisha kuwa chama hicho hakiamini katika matumizi ya nguvu kudai haki na/au kufikisha ujumbe kusudiwa. Na Lissu alikwenda mbali zaidi na kumuita Mlawa “mpumbavu.”
Yayumkinika kutanabaisha kuwa Lissu ndio mwanasiasa aliyemmaliza Mlawa, kwani tangu wakati huo, mzushi huyo amepoteza kabisa “umaarufu” aliokuwa nao, ambao nao ulichangiwa na asilimia kubwa ya wana-Chadema na baadhi ya viongozi wa chama hicho kuwa wafuasi wa matusi na unyanyasaji aliowafanyia watu mbalimbali.
Na Lissu bado ana nafasi ya kuhakikisha kuwa chama chake hakigeuki kuwa kundi la harakati, au baya zaidi, jukwaa linalotumiwa na “wanaharakati wa mtandaoni” kwa maslahi yao binafsi.
Kila afanyalo Mama Samia ni baya kwa Chadema
Kwa kutambua kuwa Mama Samia akipendwa na Watanzania wengi, “hoja za kuombea fedha kwa mabeberu kusaidia mapambano dhidi ya udikteta, nk” zitakosa mashiko, “wanaharakati wa mtandaoni” walianza kumvaa Mama Samia kabla hajatulia ofisini baada ya kuapishwa Machi 19, mwaka jana. Wakaanza kudai kuwa yeye, kama Makamu wa Rais wa Magufuli, hana tofauti na mtangulizi wake.
Wakaanzisha shinikizo la madai ya Katiba mpya, ambayo japo ni valid, lakini shinikizo hilo lina maslahi binafsi zaidi kuliko ya kitaifa (uthibitho: fuatilia vipeperushi vinavyosukuma alama ya reli kuhusu suala hilo mtandaoni vinatoka wapi).
Wanaharakati hao walifanikiwa sana kuiondoa Chadema kwenye mstari wa ustahimilivu na kukifanya chama hicho kuwa more radical, kikitumia vitisho kudai mkutano kati yao na Mama Samia, sambamba. Lakini baya zaidi lilikuwa kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kujiweka karibu na wahuni walikuwa wakimtukana Mama Samia matusi ya nguoni.
Suluhisho
Japo ingependeza kuona kesi ya Mbowe ikimalizwa “kidiplomasia” kwa Mama Samia kutumia nafasi yake na utu wake, ukweli mchungu ni kwamba lolote atakalofanya litaishia yeye kuzodolewa. Akiamua kutumia utu na uwezo wake kumaliza kesi ya Mbowe ataambiwa “dikteta kaufyata”. Akiacha sheria ichukue mkondo wake, wataendelea na wanachofanya sasa kumuita “dikteta.” Sasa kwa vile hata akifanya jema ataendelea kuonekana mbaya, basi bora asifanye lolote.
Jumapili njema