Bure Buleshi: Kozi Kadhaa Muhimu za Kompyuta

Vitu viwili. Cha kwanza, ninaandaa mtaala wa kozi ya awali ya udukuzi wa kimaadili. Niliahidi kitambo kuhusu hili lakini nilikabiliwa na vikwazo vya kilojistiki.

Lakini kabla ya kuleta kozi hiyo, ni muhimu kwa wenye nia ya kusoma kozi hiyo wakajipatia msingi wa usalama wa mtandaoni na/au uelewa kuhusu kompyuta kwa ujumla, mfano “lugha za kompyuta” kama vile python.

Pili, angalau mara moja kwa wiki, nitakuwa naweka link za kozi za bure za fani mbalimbali, hususan kompyuta. Na ikiwezekana vitabu mbalimbali.

Way forward, #BaruaYaChahali itakuwa nyenzo ya kukupatia takribani kila kitu, kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwake yaani KUHABARISHA na KUELIMISHA (na kuburudisha inapobidi).

Sambamba na maboresho hayo, ni usajili upya wa wanachama wa #BaruaYaChahali. Lengo ni kuwahudumia wale tu ambao kwa hakika wanahitaji kuhudumiwa na sio lundo la #MATAGA wanaokuja ku-copy and paste taarifa mbalimbali.

Enewei, wahi kujiunga na kozi hizi za bure kabla hazijapanda bei.

HTML, CSS, & JavaScript - Certification Course for Beginners

Practical Web Design & Development: 7 Courses in 1

Linux for Absolute Beginners

Learn HTML5 Programming By Building Projects

Basic HTML5 & CSS for beginners (Build One Project)

I hope kwa leo idadi hii inatosha. Kumbuka, takribani kozi zote za usalama wa mtandaoni zina “zero unemployment,” yaani ukihitimu huwezi kukosa kazi, iwe ndani au nje ya nchi. Na uzuri ni kwamba unaweza kutekeleza mahitaji ya mteja “remotely” yaani kwa mfano mie hapa Uskochi naweza kufanya penetration testing (uhakiki wa usalama wa mfumo wa kompyuta zako) wewe uliyepo Bariadi au Kilwa Masoko bila haja ya mie kuja huko.

Wikiendi njema.

Kocha wako,

Evarist Chahali