Bundi Bungeni Siku Ya Kupitishwa Muswada wa Vyama Vya Siasa

Uchuro au Magumashi?

Image result for spika bundi

Kwanza naomba samahani kwa kuchelewa kukutumia barua hii. Makubaliano yetu yalikuwa kwamba niwe nakutumia kila Jumatatu. Hata hivyo, majukumu yamenielemea sana na ndio maana nimechelewa kukutumia barua hii. Samahani sana.

Mada ya wiki hii inahusu matukio mawili yaliyojiri siku moja. Na yote yalijiri eneo moja. Tukio la kwanza ni taarifa ya Mtu Mfupi Job Ndugai kwamba kuna bundi alionekana bungeni jana.

Baadaye zilipatikana taarifa kwamba bundi huyo alirejea tena Bungeni

Kabla hatujaingia kwa undani kuhusuhii ishu ya bundi, hebu twende kwenye tukio jingine muhimu lililojiri jana kwenye Bunge letu.

Sasa, tukiunganisha matuki haya mawili unaweza kujiuliza

(a) Kuonekana kwa bundi asubuhi kulikuwa kunaashiria kwamba muswada huyo ni bad news?

(b) Kuonekana kwa bundi huyo kunaashiria tatizo kubwa zaidi linaloiangamiza Tanzania yetu kitambo sasa la USHIRIKINA?

Well, kwa mtazamo wangu sidhani kama ilihitajika ujio wa bundi kuashiria kuwa muswada huo uliopitishwa kuwa sheria ni more than bad news. Kama hukubahatika kuusoma, mtumishi wako nilisambaza nakala yenye tafsiri ya Kiswahili ya muswada huo.

Pengine jingine la muhimu licha ya ubaya wa muswada huo ni ubaya wa CCM na wabunge wake. Kila mara wabunge wa chama hicho wamekuwa wakitumia wingi wao bungeni kupitisha miswada mbalimbali yenye ukakasi. Tatizo kubwa la wabunge hawa ni kuweka mbele maslahi ya chama chao kuliko ya wananchi waliowapigia kura na kuwaingiza bungeni.

Muswada huo ambao sasa ni sheria ni janga kubwa kweli kweli, kama ambavyo taasisi kadhaa zilivyowatahadharishwa wabunge wetu katika BARUA HII

Kichwani wa wabunge vichwapanzi wa CCM ni kwamba chama hicho kitatawala milele, na hivyo sheria kandamizi kakam hiyo ya vyama vya siasa inatafsiriwa kuwa itawakomoa wapinzani tu.

Lakini habari mbaya zaidi ni ukweli kwamba sheria kandamizi kama hizi ndizo zitaifanya CCM iendelee kuiba kura ili kamwe isije kuwa chama cha upinzani. Maana inatambua bayana kuwa imehalalishwa ukandamizwaji wa haki za vyama vya upinzani.

Tuliache hilo kwa sasa.Turejee kwenye habari za bundi. Pengine ili nikuweke kwenye nafasi nzuri ya kunielewa, naomba ufahamu masuala kadhaa kuhusu mie mtumishi wako.

Nilipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, nilisoma kozi moja inaitwa Sociology of Religion (Sosholojia ya Dini). Nadhani inahitaji barua nzima kuweza kuelezea kwa undani kuhusu suala nyeti la USHIRIKINA.

Umemsikia Mtu Mfupi Ndugai akieleza bila uoga wala aibu kwamba “…lakini sisi Dodoma bundi wa mchana hana tatizo ila wa usiku ndo shida.” Huhitaji kuwa na uelewa mkubwa wa “tamaduni zetu” kuelewa alichomaanisha Mtu Mfupi. Mcha Mungu hawezi kuongea habari za “bundi wa usiku ndio shinda,” kwahiyo ni wazi hadi hapa unaelewa Mtu Mfupi ni wa aina gani when it comes to haya maswala ya “tamaduni zetu.”

Nimesema nilisoma Sosholojia ya Dini nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Naam, katika kozi hiyo nilipata fursa nzuri ya kuelewa kuhusu kitu tunachokiita USHIRIKINA hivi leo.

Kwa kifupi, kabla ya ujio wa Uislamu na Ukristo, babu na bibi zetu wa kale walikuwa na “dini” zao. Kwa mujibu wa Sosholojia ya Dini, neno “dini” linamaanisha imani kwa kitu flani katika jitihada za jamii kuyakabili mazingira yake. Mara nyingi imani hiyo huwa kwa kitu chenye nguvu zaidi ya uwezo wa kawaida wa kibinadamu. Iwapo nguvu hizo zipo kweli au ni za kufikirika, hilo ni suala la imani.

Uislamu uliingia “Tanzania” takriban karne ya 14 japo pia kuna maelezo kuwa inawezekana ulifika mapema zaidi kwenye karne ya 10. Ukristo uliingia “Tanzania” karne 19, takriban karne 5 (au pengine zaidi) baada ya ujio wa Uislam. Na kabla ya hapo, “dini” zilizokuwepo zilijulikana kama African Traditional Religions (ATRs) yaani “Dini za Asili za Kiafrika.”

Jamii hizo za kale zilikuwa na mgawanyiko wa majukumu kama iliyo kwa jamii za sasa, ambapo tuna serikali, bunge, mahakama, nk. Enzi hizo kulikuwa na watu waliokuwa na majukumu kama utabibu, kuomba mvua, kubariki mazao, nk.

Fast-forward miaka kadhaa baadaye, watu hawa ndio “waganga wa kienyeji” na “wachawi” tulionao zama hizi. Tofauti kati ya wale wa zama za kale na hwa wa sasa ni kwamba wale wa zama za kale walikuwa strictly kwa ajili ya mahitaji ya jamii, ilhali hawa wa zama zetu ni matokeo ya “ufisadi wa kimaadili” uliowafanya baadhi yao kutumia nguvu walizonazo “kudhuru.”

Hii ni mada ndefu na nyeti, muda ukiruhusu nitaiandika kwa kirefu zaidi, au pengine naweza kuchapisha kijitabu kidogo cha kuelezea kwa kina.

Tanzania yetu ni moja ya nchi zinazoongoza kwa imani ya USHIRIKINA. Utafiti uliofanyika mwaka 2010 - miaka TISA iliyopita - ulionyesha kuwa zaidi ya asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika USHIRIKINA.

Bila shaka, huhitaji kuwa mtafiti kubaini kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba idadi hiyo ya “waumini wa USHIRIKINA” imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi hiki cha karibu miaka 10 sasa.

Kama USHIRIKINA umetapakaa kiasi hiki, kwanii basi bado ni moja ya masuala ya siri mno? Jibu rahisi lipo kwenye picha hii hapa chini

Naam, sisi sio tu ni WANAFIKI wazuri sana ila pia twaongoza duniani. Kama ambavyo kila mtu anachukia ushoga na usagaji lakini mashoga na wasagaji ni miongoni mwa Watanzania wanoongoza kwa follwers kwenye mitandao ya kijamii, ndivyo ambavyo UNAFIKI wetu unatufanya tusiongee kwa uwazi kuhusu USHIRIKINA.

Kwa kifupi, HALI NI MBAYA SANA. Mbaya zaidi kwa sababu USHIRIKINA umeshika hatamu kwenye kada ya uongozi. Ukisikia stori kuhusu vita za kimyakimya zinazoendelea baina ya viongozi wetu -na hizi hazina vyama - basi unaweza kupoteza kabisa hamu ya hizo siasa zetu za kizushi.

Kwa kumalizia, na kwa kuzingatia nilichoongea sehemu ya mwisho wa barua hii kuhusu USHIRIKINA, yawezekana kabisa huyo “bundi wa bungeni” alikuja hapo kikazi.

Kabla sijakuaga, naomba kukufahamisha kuwa ninaanzisha “barua” nyingine ambayo itakuwa inahusu masuala ya teknolojia. Nafikiria kuiita “Chahali Na Teknolojia.” Nitakufahamisha ikiwa tayari.

Uwe na siku na wiki njema.Tukutane wiki ijayo!