Biden, Marekani na Viongozi wa Afrika waliohudhuria "US - Africa Summit 2022" wanapaswa kujisikia aibu kwa picha hii ambapo mwanamke pekee, Rais Samia, amewekwa mstari wa nyuma
Picha hii ya pamoja kati ya Rais Joe Biden wa Marekani na viongozi wa Afrika waliohudhuria “US - Africa Summit 2022” inakera kwa kila anayeguswa na nafasi ya mwanamke katika jamii.
Picha hii ni kielelezo kingine kuwa wapenda usawa - ikiwa ni pamoja na haki za wanawake - wana kazi ya ziada kukabiliana na mfumo dume kwa sababu watawala wetu wanaukumbatia …