Bashite amemdanganya Rais na Watanzania kuhusu "mawaziri wanaolipa watu ili mkuu wa nchi atukanwe mtandaoni", je Mama @SuluhuSamia ataendelea kumbeba Bashite?
Juzi, Jasusi aliwasilisha kwenu uchambuzi wa kiintelijensia wa kina kuhusu tuhuma za Bashite kwamba kuna viongozi waliwemo mawaziri wanaolipa watu wamtukane Mama Samia mtandaoni.
Uchambuzi wa kiintelijensia: tuhuma za Bashite kuwa kuna mawaziri wanalipa watu wamtukane Mama Samia ni za kweli au porojo? Ni tuhuma zake kweli au katumwa? Mabadiliko kabineti ya Mama yanukia
·
Kwa mara nyingine, Bashite ametawala anga za habari kufuatia tuhuma nzito alizotoa jana huko Arusha kwa Mama Samia wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani marehemu Edward Sokoine. Tuhuma hizo za Bashite ni kama alivyotamka kwenye video hii
Licha ya tishio lake kwamba jana angetaja majina ya viongozi ikiwa ni pamoja na mawaziri “wanaowalipa watu kumtukana Mama Samia mitandaoni”, hakuna kilichotokea (kama alivyobas…