#BaruaYaChahali, Moja ya Vijarida Bora Kabisa Duniani Kwa Lugha ya Kiswahili, Kinatimiza Mwaka wa Tatu Tangu Kianzishwe Januari 15, 2019
Kijarida chako cha #BaruaYaChahali leo kinatimiza miaka mitatu kamili tangu kianzishwe. Ni safari ngumu, kwa sababu mara tu baada ya kuanzishwa, kilizuiliwa kuonekana nchini Tanzania isipokuwa kwa kutumia VPN. Japo si vema kufurahia mabaya yanayomkuta mtu, Magufuli aliyetoa agizo hilo leo ni marehemu ilhali kijarida sio tu kipo hai bali kinaendelea kutumikia Watanzania.
Kijarida hiki kinaweza kuingia kwenye rekodi kuwa miongoni mwa machapisho machache ambayo wasomaji wake wanaona umuhimu wa kulipia inapobidi. Na katika hilo, kwanza niwashukuru nyote mlioamua kukiunga mkono kijarida hiki kwa kuwa “paid subscribers.”
Pili, ni matarajio ya mtumishi/jasusi wako kuwa kama hujajiunga na “paid subscribers,” basi birthday hii ya kijarida chako pendwa inaweza kuwa siku mwafaka kwako kufanya hivyo.
Natambua kuna wanaokerwa na utaratibu wa malipo. Lakini ukweli ni kwamba moja ya matatizo yanayosababishwa na “vitu vya bure” ni ile hali ya kuona unafanya jambo kama kujifurahisha tu. Lakini pale ambapo watu wametoa fedha zao, unakuwa sio tu na wajibu wa kuwapatia huduma waliyolipia bali pia kuna deni la kuwapatia kitu kinachokidhi matakwa yao.
Katika umri huu mpya, kijarida hiki kinaahidi kuendelea kuwatumikia kwa uadilifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kinawaletea angalau makala moja kila wiki. Pamoja na makala za uchambuzi, hususan wa kiintelijensia, kijarida hiki pia sasa kinajumuisha kozi mbalimbali, baadhi zikiwa kwa maandishi na nyingine kwa sauti (audio). Hizi zitakuwa zikiwekwa hapa mara nyingi zaidi ya makala za uchambuzi.
Basi nimalizie kwa kuwashukuru nyote mliosimama nami tangu mwanzo na mliojiunga nami baadaye pia. Shukrani zaidi kwenu mliohatarisha usalama wenu na kutumia VPN ili kusoma kijarida cha jasusi/mtumishi wenu.
Asanteni sana 🙏
Happy birthday kwa jarida na wala si kijarida kwa sababu ya content zilizomo kushiba madini ya maana.🙏🙏🙏
Happy birthday ya kijarida bora kabisa 🥳🎉🥳 tunaendelea kuchota madini na maarifa kutoka kwako Jasusi.