Barua ya Profesa Shivji kwa Rais Samia kuhusu Ngorongoro
Profesa Stahiki (Professor Emeritus), Shule Kuu ya Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Issa Shivji
Kwa heshima na taadhima pokea barua yangu nikikutumia kwa nia njema na katika kutekeleza wajibu wangu kama mwananchi na mwanazuoni kwa mujibu wa Ibara 26 ya Katiba “kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.”
Awali ya yote nakutakia maisha marefu yen…