Baada ya Kuua Vyama Vya Upinzani, Magufuli Kalilazimisha Bunge Liridhie Ufisadi Wa Sh TRILIONI MOJA UNUSU.

What's next?

Tanzania yetu inapitia kipindi kigumu zaidi ya wakati wowote ule tangu nchi yetu ipate uhuru Desemba 9, 1961. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nachi yetu, Tanzania sasa ipo chini ya utawala wa kidikteta.

Hatua hizo nne kwa mujibu wa Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ni kama ifuatavyo

Dikteta huchukua hatua kadhaa kupandikiza utawala wa imla

  1. Hupambana na Wafanyabiashara wakubwa ' matajiri ' ili kuweka matajiri wake wapya watakaokuwa msaada kwake. Rais Putin wa Russia alifanya hili vizuri sana alipochukua madaraka. Adolf Hitler yeye aliamua kuwaua wayahudi ( Jews ) kwani wakati huo Jews ndio walikuwa wanashikilia uchumi wa Ujerumani. Hapa kwetu Tanzania kwa miaka mitatu tumeshuhudia Wafanyabiashara wanakipata cha mtema kuni. Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanabambikiziwa Kodi na wakibisha wanapewa kesi zisizo na dhamana, wanatupwa jela, wananyanganywa Mali zao na wengine kufilisiwa.

  2. Huteua Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni Watu wake wa Karibu. Rais Vladimir Putin yeye alifuta kabisa chaguzi za Magavana na akateua majenerali wa jeshi na watu wa KGB badala yake. Hapa Tanzania tumeshuhudia Wakuu wa Mikoa miungu Watu wenye kufanya lolote bila kuhojiwa na yeyote. Tumeshuhudia Wakuu wa Wilaya wakifunga watu bila kufuata sheria, wakinyanganya watu mali zao na kila aina ya vituko bila kuchukuliwa hatua.

  3. Hudhibiti vyombo vya habari. Rais Vladimir Putin alihakikisha TV zote zinakuwa za Serikali kwa kutaifisha TV binafsi na ilikuwa marufuku DUMA ( Bunge la Urusi) kuonyeshwa na ni yeye tu ndiye mwanasiasa aliyepaswa kuonekana kwenye TV. Hapa Tanzania Bunge limezuiwa kuonyeshwa moja kwa moja Lakini shughuli zote za Rais Magufuli zinaonyeshwa hata kwa masuala yasiyopaswa kuonyeshwa kama vile kusaini mikataba au mashauriano na Viongozi wa dini. Sheria ya Huduma za Habari nchini imeviweka vyombo vya Habari hatarini Katika kuchapisha au kutangaza Habari zao. Serikali imeweka kanuni za leseni ili kudhibiti kuwepo na kufanya kwao shughuli zao. Waandishi wanatekwa na kupotezwa kwa Mfano Azory Gwanda wa Gazeti la Mwananchi.

  4. Hudhibiti Vyama vya Siasa. Adolf Hitler wa alifuta vyama vyote Ujerumani. Vladimir Putin alizuia mikutano ya kisiasa na kuanzisha vyama vibaraka. Hapa Tanzania, kama tulivyotabiri katika makala Hii Mwaka 2016, “ Ndio mpango utakaofanywa Tanzania kwa kuanza na kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Sheria pia itabadilishwa na kuifanya nchi ya Chama kimoja pekee, CCM”. Hili limetokea kwa tarehe 29/1/2019 Bunge kutunga sheria ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa na kumfanya Msajili wa Vyama kuwa Mdhibiti wa Vyama vya Siasa. Utekelezaji wa sheria mpya ya vyama vya siasa utapelekea ama vyama kutii maelekezo ya Serikali au kufutwa na hivyo CCM kuhodhi siasa za nchi.

Mie binafsi nimebahatika kuongea na watu mbalimbali wanaomfahamu Magufuli vizuri, kabla hajawa Rais, na takriban kila mmoja wao anaeleza bayana kuwa “kinachoendelea hivi sasa ni trela tu, picha kamili itaanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambao essentially Magufuli atakuwa mgombea pekee ndani na nje ya CCM.

Wanaomjua Magufuli wanakwenda mbali na kueleza kuwa ni mtu anayeamini kuwa yupo sahihi wakati wote na huchukulia tofauti yoyote ya kimtazamo kuwa kama vita ambayo lazima ashinde, tapeli wa kisiasa anayesifika kwa kuwatumia watu ili afikie malengo yake kabla ya kuwaangamiza (kuna mfano kuhusu jamaa mmoja aliyemwachia jimbo huko Mwanza kisha Magufuli akafanya kila jitihada kumuangamiza), na la kuogopesha zaidi, ni mtu katili ambaye hasiti kumdhuru mtu yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Waliokuwa karibu nae wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 wanaeleza bayana kuwa mara kadhaa alikuwa akitoa hitimisho lililopaswa kuwatia hofu wana-CCM wenzake, ambapo alikuwa akisema “kwanini msimuue/msiwaue tu?” Awali ilidhaniwa anasema hivyo kama mzaha lakini kadri muda ulivyokwenda ikabainika kuwa anaamini fika katika “final solution,sera ya ki-Nazi iliyopelekea mauaji ya Wayahudi takriban milioni 6.

Angalia video husika

Kibaya zaidi, Magufuli kazungukwa na lundo la marafiki zake (nasikia mwenyewe anawaita “wasiri wake”) ambao sio tu hawawezi kumwambia “Mheshimiwa hapa hauko sahihi,” lakini - na hii ni hatari zaidi - wengi wao wanafahamu “siri zake” ambazo zinamfanya awe kama mateka kwao. Unapokuwa na Rais anayemwogopa RC kwa sababu tu anafahamu habari fulani chafu kumhusu, hilo ni janga la kitaifa. Naam, wengi wa hao marafiki zake aliowajaza serikalini wanafahamu siri ambazo pindi zikiwekwa hadharani basi hata kwa udikteta hawezi kusalimika kuendelea kuongoza Tanzania yetu.

Wakati Bunge chini ya yue mbilikimo, Mtu Mfupi, likitumika kumsafisha Magufuli, hali halisi ndio huu. Mabibi na Mabwana, kumbe ile TRILIONI MOJA UNUSU ni cha mtoto…

Kwahiyo - na hili lipo ndani ya uwezo wako - mara baada ya kusoma barua hii, fanya sala/dua kuomba Mola aingilie kati janga hili linalotukabili. Waingereza wana msemo “when all hope is gone, angels may come in any form,” kwamba “pindi matumaini yote yakipotea, malaika wanaweza kuja katika namna yoyote ile.”

Na hili la “divine intervention” (kuomba Mungu aingilie kati) ni la muhimu kwa sababu kunahitajika busara kubwa katika kukabiliana na hali mbaya inayoendelea huko nyumbani. Kwa mfano, wakati Bwana Magufuli hafanyi jtihada zozote kuondoa hisia kuwa utawala wake umegubikwa na ukabila/ukanda na “unawabagua Waislamu,” ni rahisi kuibuka “watu wenye malengo yao binafsi” kuamua kutumia matatizo halisi yaliyopo na kuiingiza Tanzania yetu kwenye majanga makubwa zaidikama vile machafuko.

Nakutakia wiki njema, tukutane Jumatatu ijayo PANAPO MAJALIWA.