Barua Ya Chahali
Jasusi
AUDIO: Salamu Kutoka Kwa Mtumishi Wako
0:00
-10:20

AUDIO: Salamu Kutoka Kwa Mtumishi Wako

Naomba kukufikishia salamu hizi zilizo kwenye mfumo wa sauti (audio) ambapo naeleza kwa kifupi kuhusu mabadiliko ya muundo wa #BaruaYaChahali.

Kwa kifupi, #BaruaYaChahali “imezaa” vijarida vingine vinne, na kwa sasa mtumishi wako nitakutumia vijarida vitano kwa wiki. Ratiba ni kama ifuatavyo

#BaruaYaChahali (Jumatatu)

#ChahaliNaTeknolojia (Jumatano)

#BaruaYaShushushu (Ijumaa)

#YaliyojriWikiHii (Jumamosi)

#MtuHatari (Ijumaa)

Pia, kwa ambao hawajajisajili, usajili unaendelea HAPA na mwisho ni tarehe 15 ya mwezi huu. Nafasi zilizosalia ni chache kwa sababu lengo ni kuwa na “wanachama” (paid subscribers) 500 tu, kwa sababu (a) software ninayotumia kutuma vijarida hiyo ina masharti ya subscribers 500 , lakini pia (b) nadhani ni vema kuwa na idadi ya wastani ya watu wa kuwahudumia kuliko kuwa na lundo kubwa la watu.

Kama nilivyotanabaisha awali, muundo huo mpya utaambana na malipo kidogo ambapo “uanachama” (paid subscription) utakuwa sh 50,000 kwa mwaka (sio kwa kila kijarida bali kwa vijarida vyote vitano). Ndani ya wiki hii nitawatumia baruapepe kuwafahamisha utaratibu wa malipo utakuwaje.

Nimalizie kwa kuomba samahani kwa uduni wa kiwango (quality) cha sauti kwenye huo ujumbe wa sauti (audio).

Nakutakia siku na wiki njema

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali

Discussion about this podcast