Askofu Dkt Bagonza Amjibu Bashiru Aliyejigamba CCM Kutumia Dola Kushinda Chaguzi

Anaongea Baba Askofu Bagonza, PhD

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa
.

Kauli ya Bashiru ni hii hapa

CCM imejiandaa kushinda kihalali, na ushindi wenyewe sio wa Oktoba, ulianza kutafutwa tangu 2015,hiyo ndio tiketi yetu

Tatizo kubwa tulilokuwa nalo katika nchi yetu wananchi walishaanza kupoteza imani katika mchakato wa uchaguzi, na kuna wakati tumefikia hatua ambayo wanaojiandikisha idadi yao inakuwa kubwa lakini wanaojitokeza kwenda kupiga kura idadi inapungua hilo si jambo zuri.

Nasikia watu wanasema uchaguzi uwe huru na haki,lakini lazima tupanue tafsiri ya haki,eneo kubwa ambalo tunahitaji kuwekeza nguvu zaidi ni ushiriki wa vijana na akinamama,haya ni makundi ambayo mara nyingi hutumika na wanasiasa lakini hayanufaiki na jasho lao.

Hakuna atakayeteuliwa ndani ya CCM hasa waliyopo madarakani, bila kwenda kwenye rekodi ya utendaji wao..hakutakuwa na uteuzi wa bure.

Ukishika mbili zote zinaweza zikachomoka, aliye na dola ananufaika na dola hiyo kubaki madarakani, huo ni ukweli hata CHADEMA ikiingia kwenye dola kuiondoa kwenye dola utakuwa ni uzembe wake kwa sababu ana nafuu na faida yakuwa na dola.

Ninachoomba mimi wanasiasa wenzangu wafate sheria,maelekezo na taratibu,kwasababu nchi hii tukigeuza kuwa wakati wote ni kusema chochote na kufanya chochote..tutatafutana,ni vizuri tukawa na utaratibu wa kutujengea nidhamu.

Ni shabaha yetu kufika 50/50 lakini ni safari ndefu na ngumu lakini tutafika, hakuna kurudi nyuma, kwa ufupi ni mapambano.

Mchakato wa katiba mpya ni kiporo kilichochacha, ukila utaumwa matumbo.

Wanaosubiri sisi tulegelege kwenye kutumia dola kubaki kwenye dola watasubiri sana, hata Trump kumuondoa ngumu, kuna nafuu kubwa na faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia nguvu za dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kiweze kubaki madarakani. Aliye na dola ndiye ananufaika na dola ile kubaki madarakani, huo ni ukweli na hata CHADEMA ikiingia madarakana ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wake. Kwasababu ana nafuu na faida ya kuendelea kubakia.

Ukidhulumu mtu nikajua natafuta dola ishughulikie mtu aliyedhulumu ili nibaki madarakani, na kwakweli zamu hii ninahakika ya kushinda uchaguzi kwa sababu nitatumia dola barabara.

Ninachojua mimi hakuna mikutano iliyozuiliwa,na Polepole ni Katibu wa Itikadi na Uenezi anatangaza tuliyoyafanya ili CCM isiondolewa madarakani,sasa unataka ayatangazie wapi,chumbani?

Ilani sio Msahafu, inaweza kutekelezeka kwa kiwango fulani na si lazima iwe asilimia 100.

Hii hali ya kisiasa mnaiona,na vyama vyetu mnaviona,hivi kuna tishio ya ushindani wa kufa na kupona katika nchi hii,kiasi ambacho tuwe na uoga kwamba hautakuwa huru na haki?,mimi ntamuibia nani ana nini huyo?

Sitaki kufanya siasa za propaganda hapa, timu mnaziona? unaweza kabisa kuona ni timu gani itafunga mabao mengi? Katika mazingira ambayo kuna ushindani mkali ndio tahadhari inatakiwa kuchukuliwa,sasa jamaa anapigwa hadi mechi za mazoezi,unawasiwasi gani na refaa?

Dkt.Magufuli ametusaidia sana, kutumbua majipu, kusimamia serikali, kudhibiti matumizi mabaya ya pesa, tumetumia vizuri dola kubaki madarakani, kukusanya kodi dola hiyo hiyo ndio tunayoitumia, tulikuwa kwenye bilioni 800 sasa hivi tuko above trilioni 1

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali