Asanteni Sana

Kwanza naomba kuwafahamisha kuwa toleo la wiki hii la kijarida cha #MtuHatari kimeshatumwa kwenye inbox zenu. Lakini waweza pia kukisoma kwa KUBONYEZA HAPA.

Leo ni Juni 30, siku moja kabla ya mabadiliko ya muundo wa #BaruaYaChahali (inayojumuisha vijarida vitano kwa wiki) hayajaanza rasmi hapo kesho. Nawashuruku nyote - mliojiunga kuwa wanachama baada ya kutoa michango yenu kulingana na uwezo wenu na hata mlioamua kutochangia.

Nawashukuru kwa sababu nyote mmenipa tuzo kubwa kabisa ya kuwatumikia mara kwa siku tano kati ya saba za wiki. Hakuna tuzo kubwa maishani kama utumishi kwa jamii.

Kwa mliojiunga, tukutane kesho kwenye toleo la wiki ijayo la #BaruaYaChahali ambalo pamoja na mambo mengine litachambua kwa kina kuhusu uamuzi wa Mtu Mfupi Ndugai kumvua ubunge Tundu Lissu.

Kwa mnaoachana nasi kwa sababu moja au nyingine, milango ya kujiunga nasi itaendelea kuwa wazi kuanzia kesho japo mchango wa kuwa mwanachama utakuwa sh 100,000 kwa mwaka mzima au sh 10,000 kwa mwezi. Kwa wasomaji wa kimataifa, mchango utakuwa cha USD 75 kwa mwaka au USD 10 kwa mwezi.

Hata hivyo, bado michango inapokelewa kutwa nzima ya leo. Maelezo ni hayo hapo pichani

Kwa mlio nje ya Tanzania, michango yaweza kufanyika kwa KUBONYEZA HAPA

Nawatakia Jumapili njema.

Ndimi mtumishi wenu

Evarist Chahali