Asante sana Mheshimiwa @ridhiwankikwete kwa kusikia kilio cha wakazi wa "Watumishi Housing", Morogoro, na kuahidi kukifanyia kazi
Jana, mtumishi wako nilipokea kilio cha wakazi wa “Watumishi Housing” huko Morogoro, na niliwasilisha kilio hicho kwa njia ya makala kwenye kijarida chako hiki, nikielekeza kwa Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia utumishi wa umma.
Makala husika ni hii
Licha ya kuwa jana ni wikiendi, tena ni katika mfungo wa Mwezi Mtu…