Afikishiwe IGP Sirro: Kwanini Polisi Hawajatoa "International Arrest Warrant" Kumkamata Didier Abdallah Mlawa Aliyetoroka Kifungo Cha Miaka 15?

Tanzania yetu ni nchi ya ajabu sana. Miaka kadhaa iliyopita, aliibuka Babu Ambi na kikombe chake. Maelfu kwa maelfu ya watu walimiminika huko, na inasemekana mamia ya watu walipoteza maisha yao kwa kuendekeza kikombe badala ya tiba za hospitali.

Mkasa wa Babu Ambi hauna tofauti na ule wa DECI, ambapo maelfu kwa maelfu ya Watanzania walilizwa, kisa tamaa ya utajiri wa haraka.

Na akatokea “Dokta” Shika.

Kwahiyo siyo jambo la kushangaza kuona mtu ambaye aliibwa fedha shilingi milioni 117 jijini Dar es Salaam, kabla ya kukimbilia Arusha ambako nako akapiga shilingi milioni moja, kabla ya kukimbilia Kenya, akiibuka kuwa “msemaji wa wanyonge.”

Kilichonisukuma kuandika makala hii ni kwamba jana, mhalifu huyo alilitwiti Jeshi la Polisi la Tanzania kulitaka liachane nae na badala yake lihangaike na mie, na akaambatanisha twiti yangu moja kuhusu changamoto zilizokuwepo kabla ya Mama Samia kukabidhiwa rasmi urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo twiti yangu haikuwa na lolote la kuwapotezea muda polisi wetu.

Sasa inakuwaje mtu ambaye yeye mwenyewe anapaswa kuwa anawindwa na polisi anapata jeuri ya kuwatwiti polisi wetu? Ni kwa sababu mazingira mazima ya jinsi alivyofanya wizi wa kwanza na wa pili yalitawaliwa na uzembe wa hali ya juu.

Hebe twende kwenye mlolongo wa matukio.

11 MARCH 2013

Kigogo scania kortini akidaiwa kuiba milioni 177/-

Na Judith Michael

OFISA Utawala wa Kampuni ya Scania (T) Limited tawi la Dar es Salaam, Didier Abdallah Mlawa(38) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kughushi saini ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na kujipatia kiasi cha sh. Milioni 177

Mtuhumiwa alifikishwa mahakami hapo jana na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka Bi Ester Martin, mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Bi Janeth Minde.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alighushi saini ya mhasibu na Mkurugenzi na wa kampuni hiyo kisha kufungua akaunti benki kwa kutumia nyaraka hizo za uongo.

Mwendesha mashtaka huyo alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo kwa makosa mawili ambayo ni kughushi saini na wizi  katika kampuni ya Scania.

Mwendesha mashtaka alisema,mtuhumiwa alifanikiwa kufungua akaunti hiyo kwa kutumia majina ya wafanyakazi wastaafu waliokuwa wanafanya kazi katika kampuni hiyo.

"Mtuhumiwa alifungua akaunti hiyo Januari 10-26,mwaka huu kama mfanyakazi ambapo alifanikiwa kampuni yake kiasi cha shilingi 177.3 mali ya wafanyakazi wenzake"alisema,Mwendesha mashtaka huyo

Mtuhumiwa huyo amerudishwa rumande hadi Machi 20, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

CHANZO: Gazeti la Majira

Baadaye, mhalifu huyu alipata dhamana, na akakimbilia Arusha ambako alifanya uhalifu mwingine.

Thursday, 20 February 2014

MENEJA UAJIRI KIZIMBANI KWA KUMWIBIA MWAJIRI

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

Meneja Mwajiri wa Kampuni ya ujenzi ya Northern Engineering Ltd ya jijini Arusha, Didier Mlawa leo amefikishwa kizimbani kwa kosa la kumwibia mwajiri akiwa mtumishi kinyume cha sheria.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Mustapher Siyani, Wakili wa serikali, Ellen Rwijage alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa la hilo Agosti 30, mwaja jana.

Wakili Rwijage alidai kosa hilo ni kinyume cha kifungu sheria namba 271 kanuni ya adhabu ikisomwa pamoja na kifungu cha 265 sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

"Akiwa eneo la Mianzini jijini Arusha zilizko ofisi za kamapuni ya Northern Engineering Ltd, Mshakiwa akijua kwamba ni kosa, alimwibia mwajiri wake fedha taslimu Sh. 1 milioni kinyume cha sheria," alidai Wakili Rwijage.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao licha kutakiwa kuwa wakazi wa Jiji la Arusha wenye kazi na anuani zinazoeleweka kila mmoja alisaini hati ya dhamana ya Sh. 1 milioni.

Upelelezi wa shauri hilo halijakamilika na limeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu litakapotajwa tena.

CHANZO: Taifa Kwanza Blog

Baada ya wizi huo wa Arusha, mhalifu huyu akakimbilia Kenya. Na kukimbia huko kulipelekea ahukumiwe kwenye jela miaka 15 bila ya yeye kuwepo kortini.

Friday, August 28, 2015

Wizi wampeleka jela miaka 15

MENEJA Rasilimali Watu wa Kampuni ya Scania Tanzania Ltd, Didier Mlawa (38) amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kupatikana na hatia ya kughushi na kuiba Sh milioni 177.3.
Mlawa amehukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala bila ya yeye kuwepo mahakamani. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema kuwa mshitakiwa atatumikia kifungo hicho (adhabu isiyokwenda kwa pamoja), pia atatakiwa kurudisha kiasi hicho cha fedha kwa mwajiri wake.
Alisema kuwa mshitakiwa alitoroka baada ya kusikiliza mashahidi wawili kati ya sita na kwamba adhabu hiyo ataitumikia atakapokamatwa. ‘’Hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa na wadhamini wake itolewe na adhabu hii itaanza atakapokamatwa,’’ alifafanua.
Aliongeza kuwa kupitia mashahidi sita waliotoa ushahidi wao mahakamani hapo, walieleza kuwa mshitakiwa alighushi barua ya kufungulia akaunti benki na kwamba alipewa fedha hizo kwa ajili ya kupeleka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

CHANZO: Tupashane Habari Blog

Laiti sheria ingefuata mkondo, Jeshi la Polisi lilipaswa kutoa hati ya kimataifa ya kukamata wahalifu, yaani “international arrest warrant,” baada ya mhalifu kukwepa kifungo kwa kutorokea nje ya nchi.

Alipofika Kenya, Didier Mlawa, alifanikiwa kujenga uhusiano na Idara ya Usalama wa Kenya (NIS), na akapewa jukumu la kufanya propaganda dhidi ya Tanzania. Hata hivyo, jukumu hili lilikuwa na malengo maalum. Kwamba kwa kuiandama serikali ya Tanzania mfululizo, yatajitokeza mazingira mwafaka kwake kuonekana anawindwa na serikali, na hiyo itamrahisishia kupata hifadhi ya ukimbizi nchi za Magharibi.

Idara hiyo ya usalama ya Kenya ilimsaidia Mlawa kupata visa ya kuja hapa Uingereza kuomba hifadhi ya ukimbizi. Hata hivyo, Waingereza walikuwa hawana taarifa kuwa mkimbizi huyo is in fact a fugitive (mtu anayekimbia hatua za kisheria dhidi yake) ambaye alipaswa kuwa kifungoni.

Uzuri ni kwamba jinai haina expiry date. Kwahiyo endapo Jeshi la Polisi linamuhitaji mtu huyu kwa dhati, basi njia ya kumpata ni rahisi tu. Kwa upande mmoja wanaweza kutoa hiyo international arrest warrant na akawa “wanted” kimataifa. Lakini pengine njia rahisi zaidi ni kuifahamisha serikali ya Uingereza kuwa mtu waliyempa hifadhi kama mkimbizi is in fact mhalifu aliyekimbia kifungo cha miaka 15 jela.

Pamoja na hilo, Jeshi hilo linaweza kwenda mbali zaidi na kufahamu kuhusu Waziri mmoja wa zamani ambaye ndiye amekuwa akimpatia mhalifu huyo taarifa mbalimbali za kuichafua serikali.

Wakati mmoja, Mlawa ambaye anaweza kabisa kuwa ndani ya top ten ya watu wenye matusi kupita kiasi, aliwahi kuniita mie “snitch,” ilhali jana ni mara ya pili kwa yeye ku-snitch hadharani kuwataka polisi wanichukulie hatua. Awali alitaka wanichukulie hatua baada ya Jeshi hilo kutangaza kuwa linamuwinda.

Mdau mwenye ukaribu na Kamanda Sirro anaweza kumfikishia taarifa hii.