Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu kuondolewa kwa Balozi Mulamula kwenye uwaziri wa Mambo ya Nje, tathmini kuhusu mawaziri 'wapya.'
Nini kilichotokea? Majuzi, Oktoba 2 mwaka huu, Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko madogo ya Baraza lake la Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Rais Samia alimuondoa madarakani Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, na badala yake kumteua Dkt Stargomena Tax, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kushika wadhifa huo muhimu.
Kadhalika, Rais Samia alimteua Innocent Bashungwa, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kuchukua nafasi ya Dkt Tax huko Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Vilevile, Rais Samia alimteua Angellah Kairuki kuwa mbunge wa kuteuliwa, na kumteua kushika nafasi iliyoachwa wazi na Bashungwa.
Kwanini Balozi Mulamula ameondolewa?